Tunafanya Nini?

Kwa mujibu wa vifungu vya 88 na 97 vya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011, jukumu kuu la Mamlaka ni kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi ya malalamiko au rufaa zitokanazo na maamuzi ya maafisa masuuli katika mchakato wa kusimamia ununuzi wa Umma. Pia Mamlaka inajukumu la kusikiliza malalamiko yatokanayo na kufungiwa kwa makampuni (blacklisting of tenderers) na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Katika kutoa maamuzi Mamlaka huweza kufanya yafuatayo:

 •  Kufanya mapitio katika mchakato wa ununuzi unaolalamikiwa;
 • Kuagiza marekebisho yafanyike katika mchakato unaolalamikiwa endapo baada ya kufanya mapitio, imeonekana kuna mapungufu;
 • Kutoa ufafanuzi juu ya Sheria katika mambo ambayo yanasababisha mgogoro kati ya pande mbili zinazolumbana, yaani Taasisi ya Ununuzi na Wazabuni;
 • Kuagiza Taasisi ifanye uamuzi mwingine au Mamlaka kuubadili uamuzi wa Taasisi nunuzi na kutamka uamuzi inaoona ni sahihi; na
 • Kuagiza PPRA kuondoa zuio kwa mzabuni kutoshiriki katika Zabuni za Umma.

Madhumuni yetu

 • Kutoa nafasi kwa Wazabuni kuweza kuwasilisha malalamiko yao juu ya maamuzi au taratibu zilizotumika katika mchakato wa ununuzi wa umma pale wanapoona hawakutendewa haki .
 •  Kushughulikia migogoro inayotokea katika michakato ya ununuzi wa Umma kwa muda mfupi ili kutoathiri utekelezaji wa shughuli husika hasa miradi ya Serikali na Taasisi zake .
 •  Kutoa udhibiti wa nyongeza katika shughuli za ununuzi wa Umma (Supplemental Oversight) kupitia malalamiko ya wazabuni
 •  Kuwezesha marekebisho ya kasoro zilizojitokeza katika ununuzi wa Umma kufanyika mapema ili kuipunguzia Serikali hasara inayoweza kusababishwa na maamuzi mabaya yanayoweza kufanywa na Taasisi za
 •  Kuhakikisha ununuzi wa Umma unazingatia taratibu na miongozo iliyopo

 Dira yetu

"Chombo cha kusuluhisha migogoro ya ununuzi wa Umma kinachoaminiwa na wadau wake”

Dhima yetu

"Kutoa uamuzi wa haki na kwa wakati kwa kuzingatia utumiaji mzuri wa rasilimali zilizopo"

 Kanuni kuu

 • Kuthamini wateja
 • Uwazi na Uwajibikaji
 • Maadili na Hekima
 • Haki na Usawa
MOTO: Kutoa Maamuzi ya Haki na Kwa Wakati