NANI ANAWEZA KUWASILISHA MALALAMIKO AU RUFANI?

 Mwombaji wa Zabuni ya aina yoyote kwa mfano aliyeomba

 • Kandarasi ya ujenzi,
 • Kutoa huduma za Ushauri,
 • Kuiuzia Serikali vifaa,
 • Kutoa huduma nyinginezo,
 • Kununua kifaa kinachouzwa na Serikali kwa njia ya Zabuni

MAMBO YANAWEZA KULALAMIKIWA .

 •  Kipengele au vipengele vyenye utata au vinavyobagua Mzabuni au kuzuia isivyo halali ushiriki katika nyaraka za Zabuni (Bidding Documents) (isipokuwa vilivyoruhusiwa na Sheria)
 • Utaratibu usiokubalika katika kumpata mkandarasi, Mzabuni au Mtoa Huduma
 • Uamuzi juu ya ushindi au kushindwa katika mchakato wa Zabuni
 • Uamuzi juu ya kuingia au kusudio la kuingia
 • Kufungiwa kwa wakandarasi au watoa huduma

KUWASILISHA RUFANI KATIKA MAMLAKA YA RUFAA (PPAA).

 Pale ambapo hujaridhika na uamuzi wa Afisa Masuuli baada ya kuwasilisha malalamiko yako katika Taasisi ya Ununuzi

 Pale ambapo Afisa Masuuli ameshindwa kutoa maamuzi katika muda 

 Pale ambapo mkataba umeshasainiwa (umefungamanishwa)

Pale ambapo umefungiwa kushiriki Zabuni kutokana na Utaratibu wa Zabuni

UWASILISHAJI WA MALALAMIKO.

 A - Kwanza wasilisha malalamiko yako kwa maandishi kwa : Afisa Masuuli

 • Katibu Mkuu katika Wizara
 • Mkurugenzi wa Mkoa
 • Mkurugenzi wa Wilaya au
 • Mkurugenzi wa Halmashauri au
 • Mtendaji Mkuu wa Taasisi

 Usiporidhika na uamuzi wa Afisa Masuuli wasilisha rufani yako kwa Mamlaka Ya Rufaa (PPAA), katika muda wa siku   7 za kazi toka kufahamu uamuzi unaolalamikiwa.

B - ENDAPO Afisa Masuuli hatatoa uamuzi katika muda wa siku 7 za kazi toka ulipowasilisha malalamiko, wasilisha rufani kwa Mamlaka Ya Rufaa (PPAA)

C - ENDAPO Mkataba kati ya Mazabuni na taasisi nunuzi umeshafungamanishwa, wasilisha rufani kwa Mamlaka Ya Rufaa (PPAA)

 

ANGALIZO:

 Wasilisha rufani yako katika muda wa siku 7 za kazi toka ulipofahamu uamuzi unaolalamikia au kutopata uamuzi kutoka kwa Afisa Masuuli. Kuchelewa kuwasilisha malalamiko kutaondoa haki ya kusikilizwa .

TAARIFA MUHIMU ZINAZOHITAJIKA

 1.  Jina la Taasisi au Wizara iliyoitisha Zabuni
 2. Eleza Zabuni ipi uliyoshiriki na
 3. Eleza sababu au hoja zinazofanya ulalamike au kukata
 4. Eleza maamuzi unayotaka yafanyike na nafuu gani unataka kupewa na Afisa Masuuli au Mamlaka ya Rufaa Za Zabuni
 5. Pakua na jaza ya Rufani Appeal Form ()  

PPAA Fomu

 PPAA FOMU Na.1 (Taarifa ya Malalamiko)

 PPAA FOMU Na.2 (Majibu ya Malalamiko)

 PPAA FOMU Na.3 (Maombi ya Kuongezewa Muda )

 PPAA FOMU Na.7 (Maombi ya )

 

 

 

MOTO: Kutoa Maamuzi ya Haki na Kwa Wakati