Wasilisha Barua: barua@ppaa.go.tz  Simu:+255743505505   English  Staff Mail

PPAA2

Kuanzishwa kwa Mamlaka:

 Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma ilianzishwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 3 ya Mwaka 2001 ambapo baada ya Sheria hii kufutwa, Mamlaka iliendelezwa chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 21 ya Mwaka 2004 na kuhuishwa tena kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 baada ya ile Sheria Na. 21 ya Mwaka 2004 kufutwa.

Dhumuni hasa la kuanzishwa kwa Mamlaka hii ni kuwa na chombo mbadala cha kutatua migogoro itokanayo na michakato ya ununuzi wa Umma kwa muda mfupi zaidi tofauti na Mahakama za kawaida ili kutokuchelewesha utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Mamlaka hii pia husimamia utawala bora kupitia utatuzi wa migogoro inayowasilishwa mbele yake kwa kuhakikisha kuwa zabuni zinatolewa kwa wazabuni wenye sifa stahiki za kufanya kazi husika na hivyo kuwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha zake katika ununuzi wa Umma.

Malengo ya PPAA ni:-

  • Kutoa njia huru ambayo Wazabuni wenye malalamiko kuweza kuwasilisha malalamiko yao kuhusiana na mchakato wa ununuzi wa umma na  kuruhusu mchakato huo kuangaliwa vizuri.
  • Kuweka utaratibu utakaowezesha kushughulikia malalamiko na rufaa za ununuzi wa umma kwa kutumia njia mbadala za utatuzi wa migogoro nje ya mfumo wa mahakama na kuruhusu utatuzi wa haraka wa migogoro ili kutochelewesha utekelezaji wa mradi ya Serikali.
  • Kuruhusu hatua za marekebisho kuchukuliwa pale ambapo itabainika kuwa kulikuwa na ukiukwaji uliofanyika katika mchakato wa manunuzi.
  • Kusimamia  matumizi ya Fedha za Umma kupitia malalamiko ya Wazabuni

Majukumu ya Mamlaka

Dira na Dhamira