Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma
( PPAA)

PPAA Logo

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

14 May, 2026
TANGAZO LA MNADA WA HADHARA Wananchi wote mnatangaziwa kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), itauza kwa njia ya mnada wa hadhara vifaa mbalimbali chakavu. Mnada wa kwanza utafanyika tarehe 23 Mei 2026 katika eneo la Mkandarasi Place, Barabara ya Takwimu, Dodoma, ambapo vifaa chakavu vitakavyouzwa ni pamoja na samani za ofisi na vifaa vya TEHAMA. Aidha, mnada wa pili utafanyika tarehe 30 Mei 2026 katika Jengo la Wizara ya Fedha, 1 Mtaa wa Madaraka, Dar es Salaam, ambapo vifaa chakavu vitakavyouzwa ni pamoja na samani za ofisi na viyoyozi. MASHARTI YA MNADA Mali zote zitauzwa kama zilivyo na mahali zilipo. Malipo ni asilimia mia moja (100%) ya bei ya kifaa utakachonunua siku ya mnada. Mnunuzi atatakiwa kuondosha kifaa alichonunua siku ya mnada mara baada ya kukamilisha malipo. Ruhusa ya kuangalia mali itatolewa siku moja (1) kabla ya tarehe ya mnada. Mnada utaanza saa nne kamili (4:00) asubuhi katika kila kituo. Imetolewa na: KATIBU MTENDAJI MAMLAKA YA RUFANI YA ZABUNI ZA UMMA (PPAA)