Rufaa- Mchakato wa Ununuzi
Uwasilishaji wa Rufaa
Iwapo Mzabuni aliwasilisha malalamiko yake kwa afisa masuuli kwa mujibu wa taratibu na hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa na afisa masuuli juu ya malalamiko yake, Mzabuni anaweza kuwasilisha rufaa mbele ya Mamlaka ya Rufani ndani ya siku tano (5) za kazi toka alipofahamu jambo au uamuzi anaoulalamikia.
Mzabuni awasilishe Rufaa yake kwa kujaza PPAA Fomu Na. 1 ambayo ni Hati ya Rufaa ( Bonyeza kupakua PPAA Fomu 1) pamoja na kulipa ada ya Rufaa (Bonyeza kuona ada). Mamlaka ya Rufani itatakiwa kutoa uamuzi wake ndani ya siku arobaini (40) tangu kusajiliwa kwa Rufaa.
ANGALIZO:
- Zingatia ukomo wa muda wa uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa mbele ya Mamlaka ya Rufani.
- Mamlaka ya Rufani haishughulikii Malalamiko yatokanayo na utekelezaji wa mkataba.
Mambo yanayoweza kulalamikiwa: -
- Kukubaliwa au Kukataliwa kwa Zabuni;
- Tuzo au kusudio la kutoa tuzo;
- Vipengele visivyokubalika kwenye kabrasha la zabuni;
- Mchakato wa Zabuni usiozingatia taratibu;
- Kushindwa au kutokutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa; na
Mawasiliano: -
Katibu Mtendaji,
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma,
S.L.P 1385,
Dodoma.
Barua pepe: es@ppaa.go.tz au barua@ppaa.go.tz
TAARIFA ZA KUWASILISHA
Jina na anwani ya Wizara au Taasisi Nunuzi iliyotangaza zabuni inayolalamikiwa.
Zabuni inayolalamikiwa.
Sababu zinazopelekea rufaa / malalamiko.
Nafuu zinazoombwa.