Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma
( PPAA)

PPAA Logo

Malalamiko

Uwasilishaji wa Malalamiko

Iwapo afisa masuuli hajatoa uamuzi wake ndani ya muda wa siku tano (5) za kazi, mzabuni anaweza kuwasilisha malalamiko mbele ya Mamlaka ya Rufani ndani ya siku tano (5) za kazi tangu tarehe ambayo afisa masuuli alipaswa kutoa uamuzi. au 

Kama mkataba umesainiwa, Mzabuni atawasilisha malalamiko yake moja kwa moja mbele ya Mamlaka ya Rufani ndani ya siku tano (5) za kazi tangu alipofahamu jambo analolilalamikia.

Mzabuni awasilishe malalamiko yake kwa kujaza PPAA Fomu Na. 1 ambayo ni Hati ya Rufaa (Bonyeza kupakua PPAA Fomu 1) pamoja na kulipa ada ya rufaa (Bonyeza kuona gharama). Mamlaka ya Rufani itatakiwa kutoa uamuzi wake ndani  ya siku arobaini (40) tangu kusajiliwa kwa Malalamiko.

ANGALIZO: 

  • Zingatia ukomo wa muda wa uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa mbele ya Mamlaka ya Rufani. 
  • Mamlaka ya Rufani haishughulikii Malalamiko yatokanayo na utekelezaji wa mkataba.

 Mambo yanayoweza kulalamikiwa: -

  • Kukubaliwa au Kukataliwa kwa Zabuni;
  • Tuzo au kusudio la kutoa tuzo;
  • Vipengele visivyokubalika kwenye kabrasha la zabuni;
  • Mchakato wa Zabuni usiozingatia taratibu;
  • Kushindwa au kutokutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa; na

Wasilisha Malalamiko yako: -

Katibu Mtendaji,

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma,

S.L.P 1385,

Dodoma.

Barua pepe: es@ppaa.go.tz au barua@ppaa.go.tz

TAARIFA ZA KUWASILISHA

Jina na anwani ya Wizara au Taasisi Nunuzi iliyotangaza zabuni inayolalamikiwa.

Zabuni inayolalamikiwa.

Sababu zinazopelekea rufaa / malalamiko.

Nafuu zinazoombwa.