Majukumu ya Mamlaka
Majukumu ya Mamlaka
Majukumu ya Mamlaka:-
- Kupokea malalamiko na rufaa zitokanazo na michakato ya ununuzi wa Umma;
- Kufanya mapitio ya maamuzi ya Maafisa Masuuli kuhusiana na michakato ya ununuzi wa Umma;
- Kufanya mapitio ya uamuzi uliofanywa na Mamlaka ya Uthibiti ya Ununuzi Umma kuhusu kuwafungia wazabuni (Blacklisting of tenderers);
- Kuchukua hatua za kurekebisha pale inapoonekana kuna ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika michakato ya ununuzi.
Mamlaka ya Rufaa inafanya nini
- Kupitia malalamiko ya ununuzi wa Umma yaliyowasilishwa na kuyatatua ndani ya muda mfupi zaidi.
- Kutoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayoshindaniwa.
- Kuagiza kuchukuliwa hatua za kurekebisha pale inapobainika kuwa kulikuwa na ukiukwaji taratibu katika mchakato wa manunuzi.
- Kuagiza hatua za kurekebisha pale inapobainika kuwa pande zote hazikufuata sheria (Agizo la kutekeleza matakwa ya sheria).
- Mamlaka inaweza kuagiza malipo ya fidia stahiki kwa upande wowote. "Kifungu cha 97 (5) cha PPA / 2011 kinatoa nafuu ambazo zinaweza kutolewa na Mamlaka ya Rufaa"
Kumbuka
Rufaa au malalamiko yanayoshughulikiwa na Mamlaka ya Rufani ni yale tu yanayohusiana na mchakato wa manunuzi kabla ya utoaji wa Zabuni na yale yanayohusiana na Utoaji wa Zabuni.
Rufaa au Malalamiko yanayohusiana na utekelezaji wa mikataba yako nje ya mamlaka ya Mamlaka hii ya Rufani.