Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma
( PPAA)

PPAA Logo

Maombi ya Kutengua Uamuzi

Maombi ya Kutengua Uamuzi Uliosikilizwa Upande Mmoja (Ex-parte).

Endapo Mamlaka ya Rufani imetoa  uamuzi kwa shauri kusikilizwa upande mmoja (Mrufani, Mlalamikaji na Mleta Maombi), mrufaniwa, mlalamikiwa au mjibu maombi ndani ya siku tano kutoka tarehe ambayo uamauzi uliwasilishwa kwake anaweza kuiomba Mamlaka ya Rufani kutengua uamuzi huo.

Endapo Mamlaka ya Rufani imetoa uamuzi  kwa kumsikiliza Mlalamikaji/Mwombaji pekee, Mjibu Rufaa au Maombi ambaye uamuzi wa upande mmoja umetolewa dhidi yake, kama hajaridhika, anaweza kuomba Mamlaka ya Rufani kutengua uamuzi huo uliotolewa. Maombi la kutengua uamuzi wa upande mmoja yanapaswa kuwasilishwa kwa Mamlaka ya Rufani ndani ya siku tano kutoka tarehe ambayo uamuzi huo uliwasilishwa kwa Mjibu Rufaa au Maombi.

Maombi haya chini ya kanuni hii yatawasilishwa kwa Mamlaka ya Rufani kupitia PPAA Fomu Na. 7  ( Bofya hapa Kupakua Fomu)   pamoja na kulipa ada (Bofya hapa kuangalia ada husika).

Anwani.

Mamlaka ya Rufaa ya Ununuzi wa Umma,

S.L.P 1385,

Dodoma.

baruapepe: es@ppaa.go.tz au barua@ppaa.go.tz