Rufaa - Kufungiwa kwa Wazabuni
Uwasilishaji wa Rufaa - Kufungiwa kwa Wazabuni
Mzabuni ambaye hajaridhika na uamuzi wa PPRA wa kumfungia kushiriki katika zabuni za umma, anaweza kuwasilisha rufaa mbele ya Mamlaka ya Rufani ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe alipofahamu kuwepo kwa uamuzi huo wa kumfungia.
Mzabuni awasilishe Rufaa yake kwa kujaza PPAA Fomu Na. 1 ambayo ni Hati ya Rufaa ( Bonyeza kupakua PPAA Fomu 1) pamoja na kulipa ada ya Rufaa (Bonyeza kuona gharama). Mamlaka ya Rufani itatakiwa kutoa uamuzi wake ndani ya siku arobaini (40) tangu kusajiliwa kwa Rufaa.
ANGALIZO:
- Zingatia ukomo wa muda wa uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa mbele ya Mamlaka ya Rufani.
- Mamlaka ya Rufani haishughulikii Malalamiko yatokanayo na utekelezaji wa mkataba.
Mawasiliano: -
Katibu Mtendaji,
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma,
S.L.P 1385,
Dodoma.
Barua pepe: es@ppaa.go.tz au barua@ppaa.go.tz
TAARIFA ZA KUWASILISHA
Zabuni inayolalamikiwa.
Sababu zinazopelekea rufaa / malalamiko.
Nafuu zinazoombwa.