Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma
( PPAA)

PPAA Logo

KANUNI MPYA ZA MWAKA 2024 KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI

10 Jun, 2024

Kanuni mpya za Rufaa za Ununuzi wa Umma za mwaka 2024 zinatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni. Kanuni hizi mpya zimeundwa ili kuboresha na kuimarisha mchakato wa usikilizaji na utatuzi wa migogoro inayotokana na  michakato ya ununuzi wa umma pamoja na kuendana na mabadiliko ya sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023.

Mabadiliko Muhimu:

  1. Muda wa Kusikiliza Malalamiko:
    • Kanuni hizi zinalenga kushughulikia malalamiko kwa haraka zaidi ili kuhakikisha kuwa migogoro inatatuliwa kwa wakati na kuzuia ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya umma.Kwasasa muda wa ushughulikiaji wa malalamiko ni siku 40 toka siku 45 za awali
  2. Utaratibu wa Uwasilishaji wa Malalamiko na Rufaa:
    • Kanuni zimeweka wazi utaratibu wa jinsi ya kuwasilisha malalamiko au rufaa, ikiwa ni pamoja na nyaraka zinazohitajika na muda wa kuwasilisha.
  3. Maamuzi ya Haraka:
    • Mamlaka ya Rufaa itatoa uamuzi ndani ya siku tano za kazi baada ya kukamilisha usikilizaji wa shauri, kupunguza muda wa kusubiri maamuzi.

Kanuni hizi mpya zinatarajiwa kuongeza ufanisi na uwazi katika mchakato wa ununuzi wa umma, kuhakikisha kuwa malalamiko yanashughulikiwa kwa haki na kwa haraka, na hivyo kusaidia kuboresha utoaji wa huduma za umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa kuwa kanuni hizi zitaanza kutumika hivi karibuni, inashauriwa kwa wadau wote wa ununuzi wa umma kufahamu mabadiliko haya na kujiandaa kuyafuata.