Mafunzo ya Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Rufaa na Malalamiko
Mamlaka ya Rufani kwa kushirikiana na PPRA imeandaa semina ya mafunzo kwa wazabuni na watendaji wa taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Tanga. Semina hii inatarajiwa kufanyika tarehe 29 - 30 Mei, 2024 jijini Dar es Salaam katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) ukumbi wa Selous.
Wahusika wakuu wa mafunzo haya ni watendaji wakuu wa taasisi nunuzi pamoja na wataalamu kutoka Idara/vitengo vya Sheria, Tehama na Ununuzi/Ugavi. Hivyo tunakuomba uwaruhusu washiriki wasiozidi wanne kutoka idara/vitengo tajwa kuhudhuria mafunzo haya muhimu yatakayowawezesha kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia moduli ya kuwasilisha na kushughulikia rufaa na malalamiko kwa njia ya kielektroniki.
Aidha, Mamlaka ya Rufani imeweka ada ya uthibitisho wa kushiriki mafunzo husika ya Shilingi Elfu Hamsini tu (Sh. 50,000/=) kwa kila mshiriki. Malipo ya ada hii yafanyike kupitia control namba 995940003193 kabla ya tarehe 15 Mei, 2024. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Bi. VioletLimilabo kupitia namba ya simu 0712016223 au barua pepe: nazaeli.mkumbo@ppaa.go.tz.