Jinsi ya Kuwasilisha Maombi
Maombi yamegawanywa katika makundi makuu matatu:
- Maombi ya Kuongezewa Muda
- Maombi ya Utekelezaji wa Hukumu
- Maombi ya Kuweka Kando Uamuzi wa Upande Mmoja (Ex-parte)
1. Maombi ya Kuongezewa Muda wa Kuwasilisha Rufaa/Malalamiko
Maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha malalamiko mgogoro au rufaa nje ya muda yatawasilishwa kwa Mamlaka ya Rufani ndani ya siku tano za kazi kutoka tarehe ambayo mleta maombi alitakiwa kuwasilisha malalamiko, mgogoro au rufaa yake.
Maombi haya yatawasilishwa kwa kutumia PPAA Fomu Na. 5 (HATI YA MAOMBI) Bofya hapa Kupakua Fomu
Sababu za Maombi ya Kuongezewa Muda:
- Ugonjwa kwa kampuni ya mmiliki pekee
- Kuwa nje ya nchi
- Sababu nyingine yoyote
Kumbuka : Sababu zote lazima ziwe zimethibitishwa bila shaka yoyote.
2. Maombi ya Kuweka Kando Uamuzi wa Upande Mmoja (Ex-parte)
Endapo uamuzi umetolewa kwa shauri kusikilizwa upande mmoja , mrufaniwa, mlalamikiwa au mjibu maombi ndani ya siku tano kutoka tarehe ambayo uamauzi uliwasilishwa kwake anaweza kuiomba Mamlaka ya Rufani kutengua uamuzi huo.
Maombi haya chini ya kanuni hii yatawasilishwa kwa Mamlaka ya Rufani kupitia PPAA Fomu Na. 7 (HATI YA MAOMBI) Bofya hapa Kupakua Fomu
Maombi ya Utekelezaji wa Hukumu
Mshindi wa tuzo iliyotolewa na Mamlaka ya Rufani anaweza kuomba utekelezaji wa tuzo kwa kuwasilisha maombi kwa Mamlaka ya Rufani baada ya siku kumi na nne kutoka tarehe ya uamuzi wa Mamlaka ya Rufani.
Maombi haya yatafanyika kwa kutumia PPAA Fomu Na. 8 (HATI YA MAOMBI) Bofya hapa Kupakua Fomu
Jinsi ya Kuwasilisha Maombi Yako:
Maombi kwa barua :
Katibu Mtendaji,
Mamlaka ya Rufaa ya Ununuzi wa Umma,
S.L.P 1385,
Dodoma.
baruapepe: es@ppaa.go.tz