Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma
( PPAA)

PPAA Logo

Jinsi ya Kujitayarisha kwa Usikilizaji wa Shauri

Imewekwa: 24 Jun, 2024

 Jinsi ya Kujitayarisha kwa Usikilizaji wa Shauri

  • Wakati wa usikilizwaji wa shauri, mhusika anaruhusiwa  kuambatana na mtu yeyote au mtaalamu ambaye atamuona ni muhimu katika kufafanua hoja za shauri,Sio lazima kuambatana na Wakili, gharama za kumwalika zitalipwa na mhusika aliyemleta.

  •  Tafadhali fika na nyaraka zote zinazoweza kukusaidia katika kutetea hoja zako.

  • Wakati wa usikilizaji wa shauri wahusika hawatawasilisha hoja mpya ambazo hazikuwepo awali katika hati za shauri isipokuwa pale ambapo wameruhusiwa na Mamlaka ya Rufani.

  •  Utaratibu wa uendeshaji wa mashauri mbele ya Mamlaka ya Rufani ni rahisi na hautafungwa na masharti ya kiufundi au kanuni za lazima za ushahidi wa kimahakama.

  • Mamlaka ya Rufaa, itatoa uamuzi ndani ya siku tano za kazi baada ya kukamilisha usikilizaji wa shauri.

Zingatia: Kutokana na umuhimu wa kushughulikia malalamiko kwa haraka, Mamlaka ya Rufaa mara chache sana hupanga kuahirisha usikilizaji wa kesi.